Powered By Blogger

Sunday, February 22, 2015

Get siri nawapa alichonifunza mama.Official video VANESSA MDEE & BARNABA - SIRI



Hatimae MFloyd Mayweather atangaza siku ya mpambano kati yake na Manny Pacquiao...turupa turupa

Baada ya miaka kibao ya kukubaliana, hatimae Floyd Mayweather amekubali kuingia ulingoni na mfilipino Manny Paquiao tarehe 2 mwezi watano MGM Grand, Las Vegas.
“Niliwaahidi mashabiki wangu tutafikia muafaka na tumefikiaI,” amesema Mayweather jana (ijumaa) “tutatengeneza history tare 2. msikose.”
Mayweather ametangaza baada ya wiki kadhaa za maelewano na fununu za kama ngumi kati ya unbeaten Mayweather na eight-division champion Pacquiao zitafanyika.

mara ya kwanza walijaribu kukutana mwaka 2010, lakini mazungumzo yaliishia kati baada juu ya utaratibu wa upimaji wa madawa ya kulevya.Tangu siku hiyo kila jaribio kuwakutanisha ulingoni wawili hao liligonga mwamba kutokana na sababu mbali mbali.
lakini majadiliano yakawa kweli baada ya Pacquiao kumtandika Chris Algieri mews November mwaka jana katika mapigano yaliyofanyika Macau, na kisha kum-challenge hadharani Mayweather ulingoni.
“nimefurahi sana chamber Mayweather na mimi kuwapa mashabiki mpambano walioutaka kwa miaka mingi,” amesema Pacquiao. “Wamesubiri vya kutosha na wanastahili.”
Mazungumzo yalikuwa na utata kutokana na ukweli kuwa Mayweather ana mkataba wa kipekee na Showtime, wakati HBO wana haki na Pacquiao. Mitandao hiyo miwili imefikia maelewano kwa uhakika wa kufanya mkutano wa wito pamoja siku ya ijumaa.
Kila mtu anaehusika, wakiwemo Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wanajua mpambano huu ilikuwa utokee," Amesema Meneja mkuu wa Showtime, Stephen Espinoza. "Sote tumefurahi kuwa na uwezo kuwaleteeni tukio hili kwa mshabiki wa ndondi duniani kote."
Ken Hershman wa HBO alisema: " Manny Pacquiao na Floyd Mayweather wamekuwa wapiganaji maarufu katika mchezo wa ndondi kwa muongo mmoja uliopita na mashabikiwa ndondi duniani kote wamekuwa wakitaka kwa hamu wawili hao kukutana ulingoni. Sasa Mei 2 kila mtu anaamini itakuwa ni tukio kubwa la ndondikuwahi kutokea, mashabiki wa ndondi wapewa walichukuwa wakikiomba. Mei 2 itakuwa ni wakati sahihi kwa ajili ya mchezo wa ngumi na HBO Sports ina furaha kubwa kuwa sehemu ya tukio hili la kuvutia. "
Mpambano huo unadhaniwa kuwa mpambano tajiri katika historia ya ndondi. Unategemewa kuwa wa kishindani na kuwa na thamani ya kulipa $ 100 kwa ajili ya kulipa -kwa- mtazamo , ingawa Espinoza alisema bei Play Per Viw (PPV) "bado haijaamuliwa." Inategemewa utakwenda kimataifa na kuchukua ndondi mainstream.